KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 19, 2011

BENT AKAMILISHA SAFARI YA VILLA PARK.



Hatimae mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza Darren Bent ametimiza ndoto zake za kuitumikia klabu ya Aston Villa baada ya kufanikisha taratibu za usajili wake akitokea Stadium of Lights yalipo makao makuu ya klabu yake ya zamani ya Sunderland.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, amekamilisha usajili wa kuelekea Villa Park usiku wa kuamkia hii leo, huku uongozi wa klabu ya Aston Villa ukikubali kulipa kiasi cha paund million 18 kama ada ya uhamisho wake.

Meneja wa klabu ya Aston Villa Gerard Houllier, alimtambulisha kwa waandishi wa habari Daren Bent mara baada ya kukamilisha utaratibu wote wa usajili wake ambapo amesema usajili wa mshambuliaji huyo umevunja rekodi iliyowekwa na winga wa kimataifa toka nchini Uingereza Stewart Downing ambae alisajiliwa kwa ada ya uhamisho wa paund million 12 akitokea Middlesbrough mwaka 2009.

Gerard Houllier amesema usajili wa mshambuliaji huyo unapeleka ujumbe nje ya Villa Park kwa uthibitisho wa nini walichodhamiria kukifanya msimu huu licha ya kuwaendea kombo mpaka sasa.

Amesema kusajiliwa kwa mshambuliaji huyo pia ni sehemu ya kutimiza mipango yake ambayo aliianisha wazi wakati alipojiunga na klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu ambapo aliwaleza mabosi wake ni wachezaji wa aina gani anaowahitaji klabuni hapo kwa malengo ya kusaka mafanikio zaidi.

Kwa upande wake Daren Bent, amesema kufanikisha ndoto ya kuitumikia klabu hiyo ya Aston Villa kwake ni bahati kubwa ambayo imetimia katika wakati mufaka unaowalazimisha wachezaji wa The Villians kufanya kweli kwa minajili ya kuiokoa klabu hiyo pamoja na kujiokoa wao wenyewe kama wachezaji.

Amesema jukumu kubwa analolitambua mbele yake ni kuhakikisha anakata kiu ya mashabiki wanaoamini ujio wake ni jibu tosha kwao, kazi ambayo ameahidi kuanza kuifanya mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa ligi dhidi ya Man city.

Katika hatua nyingine Bent amekanusha taarifa zilizotolewa jana na mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Sunderland ambae kwa sasa anaitumikia klabu ya Birmingham City Kelvin Philips aliedai kwamba safari ya mshambuliaji huyo ya kuelekea Villa park inahusiana na tamaa ya fedha na si kuitumikia Aston Villa kwa moyo ulio thabit.

Amesema taarifa hizo za Philips ambazo alizitoa kama maoni yake, hazina ukweli wowote kwani endapo angehitaji pesa, hii leo angekua akiitumikia klabu ya West Ham ambayo iliyomuahidi kumlipa fedha nyingi zaidi ya atakazolipwa huko Villa Park.

No comments:

Post a Comment