KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 19, 2011

Ruud Gullit MENEJA MPYA Terek Grozny.


Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi pamoja na klabu ya HFC Haarlem , Feyenoord, PSV , AC Milan, Sampdoria pamoja na Chelsea Ruud Gullit amekubali kuingia mkataba wa kukinoa kikosi cha klabu ya Terek Grozny ya nchini urusi.

Ruud Gullit mwenye umri wa miaka 48 amekubalia kuichukua kazi hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza baada ya kuondoka kwenye klabu ya LA Galax ya nchini Marekani mwaka 2008.

Mchezaji huyo ambae anakumbukwa na wengi ulimwenguni kote kufuatia mazuri aliyoiyafanya uwanjani, amekubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kukinoa kikosi cha klabu ya Terek Grozny inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Urusi.

Hata hivyo mkataba huo uliosainiwa na Ruud Gullit, bado una mpa nafasi nyingine ya kuuboresha endapo atafikia malengo yaliyowekwa na uongozi wa klabu hiyo iliyo kusini magharibi mwa nchini Urusi.

Ruud Gullit amekabidhiwa kikosi cha klabu hiyo huku msimu wa mwaka 2011-12 ukitarajiwa kuanza March 12 mwaka huu.

Kihistoria Ruud Gullit tayari ameshaviongozi vikosi vya klabu ya, Chelsea pamoja na Newcastle Utd vya nchini Uingereza, Feyenoord ya nchini Uholanzi pamoja na Los Angeles Galaxy ya nchini Marekani kama meneja.

No comments:

Post a Comment