Siku moja baada ya uongozi wa klabu ya Balckpool kuweka ngumu na kuikataa ofa ya paund million 3.5 iliyowasilishwa huko Bloomfield Road ikitokea Aston Villa kwa ajili ya kutaka kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini Scotland Charlie Adam, hii leo uongozi wa klabu ya Liverpool umewasilisha ofa nyingine kwenye meza ya meneja Ian Holloway.
Liverpool wamewasilisha ofa hiyo ya paund million 4.5 ikiwa ni tofauti ya paund million moja zaidi ya ofa iliyowasilishwa na viongozi wa klabu ya Aston villa ambao walihitaji kumsajili Adam kwa kiasi cha paund million 3.5.
Meneja wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish amesema wamelazimika kutuma ofa hiyo baada ya kukubali uwezo wa Charlie Adam ambae mpaka sasa ameshaitumikia Blackpool michezo 61 na kupachika mabao 19 toka aliposajiliwa na klabu hiyo akitokea Ranger FC ya nchini kwao Scotland.
Amesema lengo kubwa la kutaka kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, ni moja ya mikakati yake aliyojiwekea ya kumaliza tatizo la kiungo mzuiaji ambae kwa sasa anakosekana huko anfiled.
Wakati huo huo taarifa nyingine zinaeza kwamba uongozi wa klabu ya Liverpool unajitayarisha kutuma ofa ya paund million 18 huko Amsterdam Arena yalipo makao makuu ya klabu ya Ajax Amsterdam kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uruguay Luis Alberto Suárez Díaz.
Tayari meneja wa klabu ya Ajax Amsterdam Frank De Boer ameshaeleza yu tayari kufanya biashara ya kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, endapo atapata mchezaji mwingine ambae ataziba nafasi itakayoachwa wazi.
No comments:
Post a Comment