KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, January 22, 2011

RUFAA KUSIKILIZWA FEB 2-3 MJINI ZURICH.


Rufaa za wajumbe wa kamati kuu ya shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA waliosimamishwa kwa tumuhuma za madai ya kuomba rushwa Amos Adamu na Reynald Temarii, zimeanza kusikilizwa na kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo.

Rufaa hizo zimeanza kusikilizwa baada ya kuwasilishwa majuma mawili yaliyopita huku watuhumiwa hao wawili wote kwa pamoja wakipinga adhabu iliyotolewa dhidi yao ya kufungiwa kutokujishughulisha na masuala ya soka duniani mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.

Taarifa iliyotolewa na kamati ya nidhamu ya FIFA imeeleza kuwa Amos Adamu ambae ni raia kutoka nchini Nigeria pamoja na Reynald Temarii kutoka nchini Tahiti imeeleza kuwa baada ya rufaa zao kuanza kusikilizwa, kamati hiyo imewapangia muda wa kuwasilisha utetezi wao.

Muda uliotolewa na kamati hiyo ni Februari 2-3 ambapo Amos Adamu aliefungiwa kutojishughulisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miaka mitatu pamoja na Reynald Tamarii aliesimamishwa kwa kipindi cha mwaka mmoja wametakiwa kufika mjini Zurich nchini Uswiz yalipo makao makuu ya FIFA kwa minajili ya kukamilisha zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment