Meneja wa klabu ya Blackpool Ian Holloway amegoma kumuachia kiungo wake wa kimataifa toka nchini Uingereza Charlie Adam anaetakiwa kwa udi na uvumba huko Villa park.
Holloway amegoma kutoa ruhusa kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, huku uongozi wa klabu ya Aston Villa ukiwa tayari umeshatangaza kutoa kiasi cha paund million 3.5 kama ada ya uhamisho wake.
Amesema kiungo huyo amesaini mkataba wa miezi 18 na klabu ya Blackpool na hafanani na thamani ya ofa iliyowasilishwa mezani kwake hivyo ameona ni bora aendelee kusalia huko Bloomfield Road ambapo anaamini bado kila mmoja wao anampenda na kumkubali Charlie Adam.
Amesem thamani ya mchezaji huyo ni zaidi ya paund milio 3.5 na kama itawezekana uongozi wa klabu ya Aston Villa unatakiwa kutoa zaidi ya paund million 6 kama unamuhitaji mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment