Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Norway na klabu ya Aston Villa John Carew yeye anapewa nafasi ya kujiunga na Stoke City kuongoza safu ya ushambulizi.
John Carew tayari ameshafanyiwa vipimo vya afya yake kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo huku vyombo vingine vya habari vikieleza kuwa mshambuliaji huyo amefanyiwa hivyo na klabu West Brom, hivyo atafanya chaguo la wapi ataelekea ndani ya siku kumi za usajili zilizosalia.
Carew, mwenye umri wa miaka 31, anatarajia kumaliza mkataba wake wa kuitumikia klabu ya Aston Villa mwishoni mwa msimu huu na kulikua hakuna dalili zozote za kupewa mkataba mpya na ndio maana usajili wa Daren Bent umelazimika kufanywa kwa uharaka.
Meneja msaidizi wa klabu ya Stoke City Dave Kemp amethibitisha uwezekano wa mshambuliaji huyo kuvaa jezi za rangi nyekundu na nyeupe baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati ya viongozi wa Aston Villa dhidi ya bosi wake Tony Pulis siku kadhaa zilizopita.
Kemp amesema uwezekano wa kusajiliwa kwa John Carew klabuni hapo ni mkubwa baada ya mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Senegal pamoja na klabu ya Hoffenheim ya nchini Ujerumani Demba Ba kushindwa kupita katika vipimo vya afya yake.
Amesema tayari usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ulikua umeshakamilishwa katika hatua za mwanzo na uongozi wa klabu yake ulikua umekubali kumuuza kwa kiasi cha paund million 6.
No comments:
Post a Comment