KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 13, 2011

Craig Bellamy ASHIKILIWA NA POLISI.


Jeshi la polisi mjini Cardiff linamshikilia mshambuliaji wa klabu ya Cardiff City Craig Bellamy kwa tuhuma za kuwajeruhi vijana wawili wenye umri wa miaka 20 na 26.

Ballamy anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi ambao utatoa picha kamili ya zogo hilo lililojitokeza usiku wa kuamkia hii leo kwenye mtaa wa Caroline mjini Cardiff.

Hata hivyo jeshi la polisi limeshindwa kutoa taarifa maalum ya nini chanzo cha ugomvi huo ambao tayari umeshathibitishwa na uongozi wa klabu ya Cardiff ambapo hata hivyo umesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anatarajiwa kuwepo kikosini mwishoni mwa juma hili kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza nchini Uingereza dhidi ya Norwich City.

No comments:

Post a Comment