KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, January 13, 2011

MKUU WA JESHI BADO ANA MATUMAINI.


Mkuu wa jeshi la Ashburton Grove Aresene Wenger amekiri kikosi chake hakikucheza vyema katika mchezo wa jana ambao uliwakutanisha na Ipswich Town huko Portman Road.

Wenger amesemna mchezo huo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya kombe la ligi nchini Uingereza, kwa asilimia kubwa ulitawaliwa na wachezaji wake kufuatia wapinzani wao kucheza mchezo wa kuzuia karibu muda wote, lakini mwisho wa mchezo walijikuta wakishindwa kucheza vyema na kutimiza malengo ya kupachika mabao.

Amesema Ipswich Town walitumia udhaifu wao, kwa kucheza pasi ndefu ambazo amedai ziliwazidi mbinu wachezaji wake hasa wa safu ya ulinzi na kukubali kisago cha bao moja kwa sifuri lililopachikwa nyavuni na Tamás Priskin.

Hata hivyo mzee huyo wa kifaransa ameonyesha hali ya kukiamini kikosi chake kwa kubainisha kitafanya vyema kwenye mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali utakaochezwa kaskazini mwa jiji la London Januari 25.

No comments:

Post a Comment