Hatimae ndoto za mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Senegal Demba Ba, za kucheza katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza zimetimia baada ya kusajiliwa kwa mkopo na klabu ya West Ham Utd akitokea kwenye klabu ya Hoffenheim ya nchini Ujerumani.
Mshambuliaji huyo mwemnye umri wa miaka 25 ametimiza ndoto hiyo baada ya kupata misuko suko juma lililopita pindi alipotakiwa kujiunga na klabu ay Stoke City lakini hakufanikiwa kupita katika vipimo vya afya yake.
Baada ya kukamilisha taratibu wa kujiunga na West Ham utd mshambuliaji huyo alipelekwa moja kwa moja katika uwanja wa mazoezi na akakutanishwa na wachezaji wenzake hali ambayo imeonekana kumfurahisha.
Demba Ba amesema ni faraja kubwa kwake kuwa katika mazingira tofauti na yale ya klabu ya Hoffenheim ambayo amedumu nayo kwa kipindi cha miaka sita hivyo ameahidi kufanya makubwa zaidi kufautia ushirikiano mzuri uliopo ndani ya kikosi cha The Hammers ambacho amekiri kukifuatilia mara kwa mara kinapokua uwanjani.
Demba Ba anaondoka Hoffenheim huku akiwa amepachika mabao sita msimu huu, na kusudio la kuuzwa kwake lilikuwa ni kutaka kutoa nafasi kwa Ryan Babel kupelekwa nchini Ujerumani lakini sasa dili hilo la uhamisho limeingia gizani.
No comments:
Post a Comment