Meneja wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish ametangaza kubadili msimamo na kusema winga wa kimataifa toka nchini Uholanzi Ryan Babel kwa sasa taendelea kusalia huko Anfiled.
Kenny Dalglish ametangaza kubadili msimamo huo, ikiwa ni siku chache tu baada ya kutangaza uwezekano wa mchezaji huyo kuwa mbioni kujiunga na klabu ya Hoffenheim ya nchini Ujerumani ambayo tayari ilikua imeshakubali kulipa ada ya uhamisho wake.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mapema hii leo, Kenny Dalglish amesema amelazimika kubadili msimamo huo kufuatia dili la usajili wa Ryan Babel kuvunjika huku sababu akishindwa kuiainisha wazi.
Katika hatua nyingine meneja huyo wa kimataifa toka nchini Scotland ameshindwa kuthibitisha kama ataongeza dau la kumsajili kiungo wa klabu ya Blackpool Charlie Adam kama alivyotakiwa na uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu huko Bloomfiled Road.
Ombi hilo kwa Kenny Dalglish liliwasilishwa na mwenyekiti wa Blackpool Karl Oyston mwishoni mwa juma lililopita, kufuatia ofa paund million 4 kukataliwa kwa madai haina thamani kama alivyo kiungo huyo wa kimataifa toka nchini Scotland.
Hata hivyo Dalglish amesema bado anaaminis uala la kumsajili Charlie Adam linaweza kuzungumzika kati yake na viongozi wa Blackpool hivyo amewataka waandishi wa habari kuwa na subra.
Mwishoni mwa juma lililopita kama itakumbukwa vyema meneja wa klabu ya Blackpool Ian Holloway aliikataa ofa ya paund million 3.5 iliyotumwa na uongozi wa klabu ya Aston Villa kwa minajili ya kutaka kumsajili Chalie Adam huku ikidaiwa ofa hiyo haina thamani ya mchezaji huyo aliejiunga na Seaside’s akitokea Rangers Fc.
Hii leo meneja huyo wa klabu ya Blackpool ameendelea na msimamo huo huku akidai kwamba yu tayari kumuachia Chalie Adam lakini kwa kiwango kilicho sahihi sambamba na makubaliano maalum ambayo yatamuwezesha kuendelea kucheza kila juma.
No comments:
Post a Comment