Baada ya kupokea kisago cha mabao matatu kwa sifuri ambacho kimemuondoa kwenye harakati za kusaka ubingwa wa kombe la ligi nchini Uingereza, meneja wa klabu ya Ipswich Town Paul Steven Jewell ameshindwa kujizuia kukimwagia sifa kede kede kikosi cha Arsenal ambacho kiliwafunda adabu wachezaji wake usiku wa kuamkia hii leo.
Paul Steven Jewell amesema wachezaji wa klabu ya Arsenal wanastahili sifa kubwa kutoka kwake kufuatia soka safi walilolionyesha katika mchezo huo, hatua mbayo iliwapa wakati mgumu wachezaji wake kushindwa kutimiza wajibu wa kila alichowatuma wakifanye uwanjani.
Amesema katika kipindi cha kwanza wachezaji wake walionyesha uwezo mkubwa wa kulinda ushin0di wa bao moja kwa sifuri walioupata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Prtman Road, lakini iliwauwia vigumu kuendeleza kasumba hiyo ndani ya dakika 45 za kipindi cha pili kutokana na kasi ya ajabu ya wapinzani wao.
Meneja huyo mwenye umri wa miaka 46, ameelza wazi kwamba wachezaji wake bado wanastahili pongezi kwa kuweza kuhimili upinzani mkubwa walioupata kutoka kwa Arsenal la sivyo wangeondoka na kapu la mabao huko Emirates Stadium ambapo kulifurika mashabiki wapatao 60.
Nae mkuu wa jeshi la Ashburton Grove Arsène Charles Ernest Wenger amezungumza na vyombo vya habari na kueleza kwamba tayari wametimiza wajibu wao wa kutinga katika hatua ya fainali ya michuano hiyo na kilichosalia ni kuhakikisha wanafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ya kombe la ligi.
Amesema ushujaa na kujituma kwa wachezaji wake kila siku imechua chachu kubwa kwa kikosi cha washika bunduki hao kufika hapo walipo, ambapo hata hivyo amebainisha kwamba bado anaamini watapata mafanikio makubwa zaidi endapo safari yao haitopata hitilafu yoyote.
No comments:
Post a Comment