KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, January 18, 2011

Kevin Phillips ASHANGAZWA NA MAAMUZI YA BENT.


Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Sunderland Kevin Phillips amezungumzia hisia zake kufuatia taarifa za mshambuliaji wa sasa wa klabu hiyo Darren Bent kuomba ruhusa ya kuondoka klabuni hapo.

Phillips, ambae alitumikia Sunderland kwa muda wa miaka sita (1997- 2003) amesema suala la mshambuliaji huyo kutaka kuondoka katika kipindi hiki limemshutua na hadhani kama anaondoka kwa moyo wake thabit.

Philips mwenye umri wa miaka 37, ameongeza kwamba safari ya Bent kutaka kuondoka Stadium Of Light imezingirwa na tamaa ya fedha ambapo anaamini endapo atajiunga na klabu ya Aston Villa inayodaiwa kuwa tayari kumsajili atalipwa pesa nyingi zaidi ya anazolipwa hivi sasa.

Amesema Bent hakustahili kuonyesha tabia hiyo na badala yake alitakiwa kucheza soka kwa kujituma zaidi na kuisaidia Sunderland kubaki katika mafanikio wanayoendelea kuyapata kwa sasa kwenye michezo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment