KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, January 18, 2011

Jermaine Jones AJIUNGA NA ROVERS.


Bluckburn Rovers wameendeleza mpango huo baada ya hii leo kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Marekani Jermaine Jones aliatolewa kwa mkopo wa miezi sita akitokea nchini Ujerumani kwenye klabu ya Schalke 04.

Jermaine Jones mwenye umri wa miaka 29 ameondoka nchini Ujerumani baada ya kuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Schalke 04, hatua mbayo ilisababishwa na majeraha ya ugoko aliyoyapata mwezi Novemba mwaka jana.

Meneja wa klabu ya Bluckburn Rovers Steve Kean amesema wamefikia maamuzi ya kumsajili mshambuliaji huyo, kufuatia uwezo alionao anapokua uwanjani na wana imani ataisaidia Rovers katika harakati za kutimiza malengo yaliyowekwa msimu huu.

Amesema yoyote anaemfahamu Jones atakubaliana nae kwamba mshambuliaji huyo ana vigezo vya kukitumikia kikosi chake ipasavyo, hivyo anategemea mengi zaidi kutoka kwake.

No comments:

Post a Comment