KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 26, 2011

KIKOSI CHA MABINGWA WATETEZI CHAANIKWA WAZI.


Kikosi cha mabingwa watetezi wa michuano ya mataifa bingwa barani Afrika CHAN jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kimeanikwa hadharani huku klabu bingwa barani Afrika Tout Puissant Mazembe, Englebert ikitoa wachezaji kumi na moja katika kikosi hicho.

Kikosi hicho kimetajwa kwa ajili ya kuelekea nchini Sudan kutetea ubingwa wa fainali za mataifa bingwa ya bara la Afrika zilizopangwa kuanza Feb 4-25 mwaka huu.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo Santos Mutubile Ditunga pia amewaita wachezaji sita kutoka kwenye klabu bingwa nchini Kongo mwaka 2010 Vita Club huku wachezaji watano wakiitwa kutoka kwenye klabu ya DC Motema Pembe.

Katika uteuzi huo wa wachezaji Santos Mutubile Ditunga amewashangaza wengi kwa kuwaita wachezaji wa watatu wa klabu ya TP Mazembe waliofungiwa na shirikisho la soka la Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo baada ya kugoma kujiunga na kikosi cha timu ya taifa kilichoshiriki katika michuano ya bonde la mto Nile iliyofanyika nchini Misri mwezi huu.

Wachezaji wao ni Kaluyituka Dioko, Patou Kabangu pamoja na Bedi Mbeza ambao hata hivyo inadaiwa mpaka hii leo hawajapatiwa taarifa za kimaandishia ambazo zinathibitisha kifungo chao.

No comments:

Post a Comment