KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 17, 2011

Lawrence Siphiwe Tshabalala HUYOOOO ULAYA.


Mshambuliaji wa pembeni wa kimtaifa toka nchini Afrika kusini, pamoja na klabu ya Kaizer Chiefs Lawrence Siphiwe Tshabalala leo anatarajia kuanza majaribio na klabu ya Nottingham Forest ya nchini Uingereza.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 26 aliefunga bao la kwanza kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka jana, ameelekea nchini Uingereza baada ya kuwavutia viongozi wa Nottingham Forest ambao kwa muda mrefu walikua wakimfuatilia kupitia michezo ya klabu yake.

Wakala wa Siphiwe Tshabalala, Jazzman Mahlakgane amesema mbali na klabu hiyo ya ligi daraja la kwanza nchini Uingereza kutimiza lengo la kumjaribu mchezaji wake, bado kuna vilabu vingine nchini humo vilishavutiwa na uchezaji wa winga huyo.

Mahlakgane, amesema endapo Siphiwe Tshabalala atafanikiwa katika majaribio hayo uongozi wa klabu ya Nottingham Forest umeshatangaza kuwa tayari kutoa kiasi cha paund million 1.5 kama ada yake ya uhamisho kutoka nchini Afrika kusini hadi Uingereza.


No comments:

Post a Comment