Safari wa kiungo wa kimataifa toka nchini Afrika kuisni Steven Jerome Pienaar ya kutoka Goodson Park kuelekea jijini London imeiva baada ya meneja wa klabu ya Everton David Moyes kuthibitisha kuikubali ofa ya klabu ya Chelsea na kuimwaga ofa ya klabu ya Tottenham Hotspurs.
Moyes ametoa uthibitisho wa kuikubali ofa hiyo, mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana wa ligi kuu dhidi ya Liverpool ambapo amesema imemlazimu kuikubali ofa ya klabu ya Chelsea kufuatia utaratibu ulioanishwa kupitia vilelezo alivyovipata huku sababu kubwa ya kuikataa ofa ya Spurs akisema haieleza wazi nini matakwa yao kwa mchezaji huyo.
Hata hivyo Moyes amesema bado watampa nafasi Steven Pienaar kukaa meza moja na viongozi wa klabu ya Chelsea kujadili masuala mbali mbali ya kimkataba ambayo kwa sasa hakubaliani nayo na inaaminiwa mazungumzo hayo yatafikia muafaka.
Sababu ya kuuzwa kwa Steven Pienaar ni kufuatia mkataba wake wa kuitumikia klabu ya Everton kutarajia kufikia kikomo mwishoni msimu huu, na tayari ameshagoma kusaini mkataba mpya kwa lengo la kuhitaji maslahi zaidi ambayo uongozi wa klabu hiyo haupo tayari kuyalipa.
No comments:
Post a Comment