KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 10, 2011

MARADONA KUELEKEA UINGEREZA.


Gwiji wa soka toka nchini Argentina Diego Armando Maradona anatarajia kuelekea nchini Uingerezqa mwezi ujao kwa lengo la kuvitega vilabu vya soka nchini humo ambavyo vitaonyesha nia ya kutaka kumuajiri kama meneja.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu na gwiji huyo aliekiongoza kikosi cha taifa lake kwenye fainali za kombe la duniani mwaka jana huko nchini Afrika kusini, La Nacion pamoja na Clarin zimeeleza kuwa haifahamiki Maradona atakua nchini Uingereza kwa kipindi gani lakini uhakika wa safari ya kuelekea nchini humo upo mwezi Februari mwaka huu.

Muda mchache baada ya taarifa hizo kutolewa Maradona mwenye umri wa mika 50, ambae yupo mapumzikoni nchini Uruguay katika mji wa Punta del Este aliwathibitishia waandishi wa habari juu ya safari yake ya kuelekea nchini Uingereza.

Maradona toka alipotimuliwa kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Argentina mara baada ya kuondolewa kwenye fainali za kombe la dunia na timu ya taifa ya Ujerumani, bado hajarejea tena katika tasnia ya mchezo huo kama kocha.


No comments:

Post a Comment