KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 10, 2011

Ryan Babel AMUAIBISHA Howard Webb.


Winga wa kimataifa toka nchini Uholanzi Ryan Babel amewaomba radhi mashabiki wa soka la nchini Uingereza pamoja na muamuzi Howard Webb kufuatia picha aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twiter mara baada ya mchezo wa Liverpool na Man utd kumalizika hapo jana.

Ryan Babel imemlazimu kuomba radhi kufuatia kigezo cha picha aliyoiweka kwenye mtandao wa Twiter ambayo inamuonyesha muamuzi Howard Webb akiwa amevaa jezi ya Man utd ambayo iliashiria ni shabiki mkubwa wa klabu hiyo ya Old Traffold.

Sababu kubwa inayodhaniwa hadi kufikia hatua kwa winga huyo kuweka picha hiyo ni kuchukizwa na maamuzi yaliyotolewa jana na Howard Webb ambae aliizawadia Man utd penati katika dakika ya kwanza sambamba na kumuonyesha kadi nyekundu nahodha na kiungo wa Liverpool Steven Gerrard.

Sakata hilo, kwa sasa linachunguzwa na chama cha soka nchini Uingereza na kuna uwezekano mkubwa kwa winga huyo kuadhibiwa na chama hicho kwa kosa hilo alilolifanya.


No comments:

Post a Comment