Kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi Mark Peter Gertruda Andreas van Bommel, hii leo ametoa mkono wa kwaheri kwa wachezaji na viongozi wa klabu ya Bayern Munich, baada ya kukamilika kwa dili la kuelekea nchini Italia kujiunga na mabingwa wa zamani wa barani ulaya Ac Milan.
Mark van Bommel ameondoka mjini Munich huku akionyesha bado alikua na mapenzi ya dhati na klabu ya Bayern Munich ambayo ilimsajili mwaka 2006 akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Hispania Fc Barcelona.
Sababu kubwa iliyomng’oa kiungo huyo huko Allianze Arena ni mkataba wake ambao ulitarajiwa kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu na hakukuwa na dalili zozote za kuongezewa mkataba mwingine hivyo uongozi wa Bayern Munich umeona ni bora umuuze kwa minajili ya kupata faida.
Hata hivyo bado haijaelezwa ni kiasi gani cha fedha kilichotolewa na uongozi wa klabu ya Ac Milan kama ada ya uhamisho wa Mark van Bommel, ambae ameahidi kuendeleza shughuli ya kucheza kwa kujituma akiwa na klabu yake mpya iliyo na maskani yake makuu mjini Milan nchini Italia.
Mwenyekiti wa klabu ya Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amemtakia kila la kheri Mark van Bommel katika utaratibu wa maisha mapya akiwa na klabu ya AC Milan ambayo kwa sasa inashikilia usukani wa ligi kuu ya soka nchini Italia *SIRIE A*.
No comments:
Post a Comment