KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, January 25, 2011

Arsenal Vs Ipswich Town


Meneja wa klabu ya Ipswich Town Paul Jewell amesema usiku huu kikosi chake kinaelekea Emirates Stadium huku kikitambua nini kinachohitajika katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya kombe la ligi nchini Uingereza Curling Cup.

Paul Jewell aliekabidhiwa kikosi cha klabu hiyo ya ligi daraja la kwanza baada ya kutimuliwa kazi kwa aliekuwa meneja huko Portman Road Roy Kean, ameeleza wazi kwamba suala kubwa usiku huu ni kulinda ushindi wao wa bao moja kwa sifuri walioupata majuma mawili yaliyopita pale walipokutana na Arsenal katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali.

Amesema katika mchezo huo wapinzani wao waliwadharau na walitumia udhaifu huo kuwashinda kwa idadi ya bao moja kwa sifuri lililopachikwa wavuni na Tamas Priskin katika dakika 10 za mwisho.

Hata hivyo Jewel alieikacha Derby County kwa kutangaza kujiuzulu kufutia matokeo mabovu yaliyokua yakimuandama amesema bado ataendelea kutumia mfumo wa kujihami na kufanya mashabulizi ya kushtukiza kama ilivyokua katika mchezo wa kwanza ambapo mfumo huo uliwasaidia kupata ushind.

Lakini pamoja na kutoa tambo hizo Jewel amekiri kuutambua uwezo mkubwa wa Arsenal wanapokua nyumbani huku akikumbushia kisago cha mabao matatu kwa sifuri kilichotolewa kwa Wigan Atheletic mwishoni mwa juma lililopita katiak mchezo wa ligi.

Wakati huo huo meneja wa klabu ya Arsenal Arsène Charles Ernest Wenger amesema anajisikia mwenye furaha kuendelea kuwepo ndani ya michuano minne msimu huu hadi kufikia kipindi hiki cha mwezi januari hivyo anaamini hali hiyo inaendelea kuwajenga wachezaji wake kucheza kwa kujituma zaidi kila panapokucha hatua mbayo ameeleza itaendelea kuonekana usiku huu.

Amesema lengo lake ni kuhakikisha anashinda mchezo wa hii leo na anaamini hilo linawezekana hivyo amewataka mashabiki wa klabu hiyo kusubiri na kuona ni vipi kikosi cha klabu yao kinavyopenya katika hatua ya nusu fainali na kuelekea fainali.

No comments:

Post a Comment