Meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Redknapp amesema hayupo tayari kuachia kwa namna yoyote ile kiungo wa kimataifa toka nchini Croatia Niko Kranjčar ambae kwa juma hili amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kujiunga na klabu ya Wolfburg ya nchini Ujerumani.
Redknapp amesema hawezi kukubaliuana na hali ya kuondoka kwa kiungo huyo, kwani bado anamuhitaji kikosini kwa udi na uvumba hasa katika kipindi hikia mbacho kikosi chake kinabiliwa na micheza zaidi ya mmoja ndani ya juma moja.
Amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 bado ana uwezo mkubwa wa kuitumikia Spurs ambayo inahitaji usaidizi mkubwa wa mchezaji kama huyo kwa ajili ya kutimiza malengo yaliyowekwa huko White Hert lane.
Amesema kwa sasa wanakabiliwana michezo ya ligi kuu, michezo ya kombe la FA sambamba na michezo ya hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya mabingwa zamani AC Milan ambao wataanzia nyumbani Sun Siro na kisha kumalizia mchezo wa pili jijini London.
No comments:
Post a Comment