Meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Michelangelo Ancelotti amekataa kata kata kulizungumzia suala la mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Hispania pamoja na klabu ya Liverpool Fernando José Torres Sanz ambae toka jana amekua anahusishwa na taarifa za kutaka kuelekea Stamford Bridge.
Ancelotti amegoma kulizungumzia suala la mshambuliaji huyo hukua kidai, kuiheshimu sana klabu ya Liverpool yenye haki na mchezaji huyo kwa hivi sasa kufuatia mkataba unaendelea kumlinda Fernando José Torres Sanz huko Anfiled.
Amesema kwa sasa ana haki aya kuulizwa na vyombo vya habari juu ya kikosi chake ambacho na haki zote za kukizungumzia wakati wowote ule lakini katu hatozungumza suala la mchezaji mwingine ambae hausiani na The Blues.
Meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italia pia amegoma kuzungumzia suala la beki wa kimataifa toka nchini Brazil pamoja na klabu ya benfica ya nchini Ureno David Luiz Moreira Marinho ambae jana jioni dili lake la kutaka kujiunga na klabu ya Chelsea lilitangazwa kuvunjika.
No comments:
Post a Comment