Beki wa kimataifa toka nchini Argentina Pablo Javier Zabaleta Girod amesema meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini ndie chanzo cha kuondoka kwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Togo Emmanuel Sheyi Adebayor.
Pablo Javier Zabaleta Girod amesema kulikua na dalili zote zinazoonyesha kwamba Mancini hakumuhitaji Adebayor katika kikosi chake na ndio maana alishindwa kumpa nafasi ya kuitumikia klabu hiyo ipasavyo na mwisho wa siku alidiriki kumpa nafasi ya kutosha mshambuliaji Carlos Tevez.
Amesema yeye binafsi anaukubali uwezo wa Adebayor na ilimuuma sana kuona hapatiwi nafasi ya kutosha kila walipokua katika harakati za kusaka point tatu kwenye michuano ya ndani ya Uingereza pamoja na ile ya kimataifa.
Mbali na kutoa sababu ya kunyimwa nafasi huku Carlos Teves akionekana kama mfalme wa kubembelezwa kila kukicha, Zabaleta ameongeza kuwa, Mancini aliendelea kumdhihirishia mshambuliji huyo kutoka barani Afrika ahitajiki klabuni hapo pale alipomsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Bosnia Edin Dzeko.
Adebayor, mwenye umri wa miaka 26, tayari amejiunga na kikosi cha Real Madrid kwa mkopo huku akifanikiwa kupita katika vipimo vya afya, na mshahara wake kwa juma akiwa huko Estadio Stantiago Bernabeu utakua akilipwa paund 160,000.
No comments:
Post a Comment