Uongozi wa klabu ya Sunderland umewashiwa taa ya kijani kwa minajili ya kufanya mazungumzo na kiungo wa kimataifa toka nchini Ghana pamoja na klabu ya Inter Milan Sulleyman Ali "Sulley" Muntari.
Taa hiyo ya kijani imewashwa na uongozi wa klabu yake ya sasa ya huko nchini Italia na inategemewa kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, huenda akajiunga na klabu ya Sunderland kabla ya tarehe ya mwisho ya kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
Muntari anapigiwa chapuo la kutaka kuelekea huko Stadium Of light kufuatia kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza cha mabingwa wa soka barani Ulaya Inter Milan, hali ambayo inamsukuma kuondoka huko Stadio Giuseppe Meazza.
Endapo dili la Sulleyman Ali "Sulley" Muntari litafana, klabu ya Sunderland itakua inawamiliki wachezaji watatu kutoka nchini Ghana ambapo kwa sasa klabu hiyo ya nchini Uingereza inammiliki Asamoah Gyan pamoja na John Mensah.
Wakati huo huo kiungo wa kimatauifa toka nchini Ghana na klabu bingwa nchini Italia Inter Milan Sulleyman Ally Sulley Muntari amewasili mjini Newcastle kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo na viongozi wa klabu ya Sunderland.
Kiungo huyo amewasili mjini humo baada ya kuwashiwa taa ya kijani na uongozi wa klabu yake ambao upo tayari kumuuza kwa mkopo katika kipindi hiki cha dirisha dogo kufuatia kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza ch The Nerazzurri.
No comments:
Post a Comment