Ndoa ya uongozi mpya wa klabu Liverpool na Roy Hodgson hii leo imevunjika rasmi baada ya meneja huyo wa kimataifa toka nchini Uingereza kuamua kubwaga manyanga mishale ya mchana kwa majira ya saa za Afrika mashariki ili hali huko jinni Liverpool ilikua ni mishale ya asubuhi ya saa tano.
Hodgson, mwenye umri wa miaka 63, amemua kuondoka huko Anfield, baada ya kushindwa kuafikiana na uongozi mpya wa klabuhi hiyo ambao ulimtaka ajihukumu mwenyewe kupitia mazungumzo rasmi yaliyokua yakiendelea tangu juzi.
Taarifa zimeeleza kuwa Hodgson alirtakiwa kujibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na mabosi wake ambayo angekubaliana nayo yangemfunga na kujikuta wakati wopwote akifukuzwa klabuni hapo, lakini ameona ni bora ajiondoe mwenyewe kabl tya kauli ya kumtimu haijatolewa.
Kuondoka kwa meneja huyo aliekiwezesha kikosi cha Fulham kufika hatua ya faionali ya michuano ya kombe la ligi ya barani Ulaya msimu uliiopita, kunatoa nafasi kwa gwiji wa zamani wa Liverpool Kenny Dalglish kukabidhiwa mikoba ua kukiongoza kikosi cha The Reds hadi mwishoni mwa msimu huu.
Hodgson anaondoka klabuni hapo huku akiwa na kumbu kumbu mbaya ya kichapo cha mabao matatu kwa moja dhidi ya Blackburn Rovers kwenye mchezo uliounguruma siku ya jumatano ya juma hili.
Mpaka hii leo Roy Hodgson anaondoka Anfiled tayari alikua meshakiongoza kikosi chake katika michezo 20 ya ligi ambapo kati ya hiyo ameshinda michezo saba, ametoka sare michezo minne na ameshinda michezo tisa, hali ambayo imekifanya kiksoi cha Liverpool kukamata nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi.
No comments:
Post a Comment