KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, January 8, 2011

SAGNA ATOBOA SIRI YA KUPEWA KADI NYEKUNDU.


Hatimae beki wa kimataifa toka nchini Ufaransa Bacary Sagna amevunja ukimya na kueleza nini kilichosababisha malumbano kati yake na beki wa klabu ya Man city Pablo Zabaleta pale klabu zao zilipokutana kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza kati kati ya juma hili huko jijini London.

Bacary Sagna amevunja ukimya huo na kumaliza hisia za mashabiki wa soka ulimwenguni kote waliofuatilia mchezo wa Arsenal dhidi ya Man City ambapo wengi wao walijiuliza ni hatua ipi iliyomfanya beki huyo mwenye umri wa miaka 27, kulumbana na Zabaleta baada ya kuchezewa ovyo pembezoni mwa uwanja.

Sagna amesema alilazimika kuzusha malumbano hayo kufuatia tusi la nguoni alilotukanwa na Zabaleta kwa lugha ya kihispaniola ambayo amedai anaifahamu uzuri kwa kuisikia na kuizungumza pia.

Amesema mbali na kuchukizwa na tusi hilo pia, amekua akifanyia rafu za kipuuzi na wachezaji wengi na hakuna taratibu zozote zinazochukuliwa na waamuzi wanaochezesha michezo ya Arsenal hivyo alipandwa na hasira baada ya kujiuliza kwa muda mrefu kwa nini iwe kwake kila siku.

Hata hivyo Sagna amewataka radhi mashabiki wa soka ulimwenguni kote wanaomkubalia sambamba na wale wa klabu yake ya Arsenal kwa kosa hilo ambalo sasa linamkosesha michezo mitatu mfululizo ambapo adhabu hiyo imeanza katika mchezo wa leo.

Wakati Sagna akiomba radhi kwa mashabiki wake, chama cha soka nchini Uingereza jana kimetengua adhabu ya Zabaleta ya kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia kosa la kulumbana na beki huyo wa kifaransa siku ya jumatano.

Zabaleta amefutiwa adhabu hiyo baada ya uongozi wa klabu yake ya Man City kukata rufaa ya kupinga maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya mchezaji huyo wa kimataifa toka nchini Argentina.

No comments:

Post a Comment