KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, January 7, 2011

Sepp Blatter ATOA MATUMAINI YA 2022.


Fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 zitakazofanyika nchini Qatar, huenda zikachezwa mwezi januari kufuatia hali ya hewa ya ukanda wa nchi za falme za kiarabu.

Hisia hizo zimeibuka baada ya maelezo yaliyotolewa na raisi wa shirikisho la soka duniani kote FIFA Sepp Blatter kabla ya kuanza kwa fainali za mataifa ya barani Asia ambazo zinaanza hii leo nchini Qatar.

Blatter amesema upo uwezekano mkubwa wa fainali hizo za kombe la dunia zikacheza katika msimu wa majira ya baridi ambao hupatikana katika kipindi kama hiki ambacho kinashuhudia fainali za barani Asia zikichezwa huko nchini Qatar.

Amesema bado wanafikiria ombi lililowasilishwa kwao juu ya kubadilishwa kwa utaratibu wa muda wa kuchezwa kwa fainali hizo za kombe la dunia, lakini akasisitiza kwamba ombi hilo lina umuhimu mkubwa.

Kiwango cha joto kuanzia mwezi June hadi Julai katika nchi za falme za hufikia nyuzi joto 40, hali ambayo inahofiwa kuleta karaha kwa nchi shiriki pamoja na mashabiki watakaofurika huko nchini Qatar kushuhudia fainali za kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment