KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 5, 2011

TONY PULIS AMKUBALI NANI.


Mfungaji wa bao la pili na la ushindi katika mchezo wa jana Luís Carlos Almeida da Cunha NANI amemwagiwa sifa kede kede na meneja wa klabu ya Stoke City Tony Pulis ambae alishindwa kujizuia kumzungumza winga huyo wa kimataifa toka nchini Ureno.

Tony Pulis amesema winga huyo mwenye umri wa miaka 24, jana ameonyesha uwezo mkubwa wa kisoka hali ambayo amekiri iliwauwia vigumu wachezaji wake kumkaba kila ilipotakiwa kufanya hivyo.

Amesema ushirikiano wa Louis Nani pamoja na Ryan Giggs nao ulichangia kwa kiasi kikubwa kwa kikosi chake kushindwa kutimiza lengo la kuibanjua Man Utd nyumbani kwao hivyo hana namna ya kushindwa kumpa tano mchezaji huyo ambae alifunga bao mashuhuri lililoipigilia misumari Man Utd kileleni.

Matokeo mengine ya michezo iliyochezwa jana ni pamoja na;

Bloomfield Road
Blackpool 1-2 Birmingham

Craven Cottage
Fulham 3-0 West Brom

No comments:

Post a Comment