KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 5, 2011

Faouzi Benzarti AREJESHWA KIBARUANI.


Hatimae shirikisho la soka nchini Tunisia limemtangaza mbadala wa alikua kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo The Carthage Eagles Bertrand Marchand ambae alitimuliwa kazi mwishoni mwa mwaka uliopita.

Shirikisho la soka nchini humo limemtangaza Faouzi Benzarti kwa mara nyingine tena kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tunisia ambayo ni miongoni mwa mataifa yanayosakla nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Afrika mwaka 2012.

Faouzi Benzarti ameteuliwa kushikwa wadhifa huo, huku wengi wakimkumbuka kwa mazuri aliyoyafanya ambapo moja ya mazuri hayo ni kuifikisha Tunisia kwenye fainali za mataifa ya bara la Afrika za mwaka 2010, kabla ya timu kukabidhiwa na Bertrand Marchand mara baada ya kumalizika kwa fainali hizo huko nchini Angola.

Mkataba wa Benzarti unaonyesha atakuwa na jukumu la kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tunisia hadi mwishoni mwa mwaka huu huku jukumu kubwa linalomkabili ni kuhakikisha anaiwezesha The Carthage Eagles kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2012.

Tunisia imepangwa katika kundi la 11 katika harakati za kusaka nafasi ya kucheza fainali za barani Afrika mwaka 2012 ambapo kundi hilo lina timu za nchi kama Botswana, Togo pamoja na Chard.

Kabla ya kuteuliwa kurejea tena katika nafasi hiyo Benzarti alikua akikifundisha kikosi cha klabu bingwa nchini Tunisia Esperance ambacho alifanikiwa kukifikisha kwenye hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo walikutana na mabingwa wa michuano hiyo TP Mazembe kutoka jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

No comments:

Post a Comment