Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Hispania Fernando José Torres Sanz huenda akaondoka huko Anfiled na kuelekea Stamford Bridge yalipo makao makuu ya klabu ya Chelsea inayomilikiwa na taykun wa kirusi Roman Akadyevich Abramovich.
Safari ya mshambuliaji huyo mwenye umti wa miaka 26, inapewa nafasi kubwa baada ya uongozi wa klabu ya Liverpool, kueleza wazi kwamba Torres yu huru kuondoka endapo uongozi wa klabu ya Chelsea utakua tayari kutoa kiasi cha paund million 50 kama ada ya uhamisho wake.
Mbali na kutoa utaratibu huo wa safari ya Torres pia uongozi wa klabu ya Liverpool umesema endapo Chelsea watashindwa kutoa kiasi cha paund million 50 bado wana nafasi nyingine ya kukamilisha usajili wa mspaniona huyo kwa kutoa kiasi cha paund million 40 pamoja mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ufaransa Nicolas Sebastien Anelka (Abdul-Salam Bilal).
Safari ya Torres inapewa kipaumbele katika kipindi hiki kufuatia mkataba wake kueleza wazi kwamba endapo Liverpool itashindwa kufuzu kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya msimu ujao, ana ulazima wa kuondoka klabuni hapo kwa ada ya uhamisho wa paund million 50.
Taarifa hizo za Liverpool kuanika wazi ada ya uhamisho wa Torres zimetolewa huku dirisha dogo la usajili likitegemewa kufungwa mishale wa saa 11:59 usiku wa hii leo kwa saa za barani Ulaya.
No comments:
Post a Comment