Sakata lingine la usajili, linatokea huko City Of Manchester ambapo imedaiwa kwamba beki wa pembeni wa klabu ya Man city Jerome Boateng amekua mstari wa mbele kuushawishi uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha unamsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Bosnia pamoja na klabu ya Wolfburg Edin Dzeko.
Jerome Boateng anadaiwa kufanya hivyo huku akimwagia sifa kem kem mshambuliaji huyo kwa kudai kwamba atakisaidia kikosi cha Man City ambacho kinahitaji wachezi wanaojua shughuli kama Dzeko ambae atasaidiana na wachezaji wengine klabuni hapo katika suala la kutimiza malengo yaliyowekwa.
Beki huyo wa kimataifa toka nchini Ujerumani, amenukuliwa akisema anamfahamu fika mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, kufuatia umahiri wake anaouonyesha akiwa uwanjani ambapo pia amekiri kuutambua vilivyo umahiri huo wakati alipokua akiitumikia klabu ya Humburg kabla hajajiunga na Man city.
Uongozi wa Man City tayari umeshajaribu kumsajili Edin Dzeko mwishoni mwa mwaka jana lakini hatua hizo zilionekana kufifia baada ya uongozi wa Wolfburg kuhitaji kiasi kikubwa cha pesa kama ada yake ya usajili.
No comments:
Post a Comment