KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 3, 2011

TAARIFA ZA GAUCHO ZAKANUSHWA.


Uongozi wa klabu ya Blackburn Rovers umekanusha taarifa za kutaka kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini Brazil na klabu ya AC Milan ya nchini Italia Ronaldo de Assís Moreira *Ronaldinho Gaucho* ambae kwa sasa yu mbioni kurejea nyumbani kwao kuitumikia klabu yake ya zamani Gramio.

Wamiliki wa klabu hiyo ya nchini Uingereza wamekanusha taarifa hizo baada ya kujitokeza katika vyombo mbali mbali vya habari nchini humo ambavyo vimedai viliichukua taarifa hiyo kupitia mitandao ya Facebook pamoja na Twitter ambapo inadaiwa kwenye kurasa zinazomilikiwa na wamiliki hao ziliandikwa taarifa za kutaka kusajiliwa kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30.

Taarifa za kukanusha uvumi huo, zimetolewa hii leo na mkurugenzi wa klabu ya Rovers Venkatesh Rao ambapo amesema usajili kwa kiungo huo haupo na wala hautawezekana.

No comments:

Post a Comment