KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 5, 2011

WENGER AWADHARAU WANAIKIBEZA KIKOSI CHAKE.


Kaskazini mwa jiji la London yalipo makao makuu ya klabu ya Arsenal, kamanda wa kikosi cha Ashburton Grove, Arsene Wenger ametamba kikosi chake msimu huu kimekata ngebe za wale wote waliokua wakikiondoa kwenye ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Wenger ameyasema hayo huku akiendelea kutoa mwanya kwa kila shabiki duniani kuendelea kutoa mawazo yake binafsi juu ya kikosi chake lakini ukweli ni kwamba bado anaamini The Gunners msimu huu wamebadilika kwa kila hatua.

Amesema wanakwenda kucheza mchezo wa usiku huu dhidi ya Man City wakiwa katika hatua nzuri ya kiuchezaji hivyo hana shaka na wachezaji wake ambao ameshawasisistiza kuboresha mazingira ya ushindi wanapokua katika ardhi ya nyumbani kama wanavyofanya katika viwanja vya ugenini.

Nae meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini ameonyesha kukubaliana na maneno ya mpinzani wake kwa kueleza kwamba kikosi cha Arsenal kipo katika kiwango cha hali ya juu na hilo limempa nafasi ya kuangalia ni vipi anakiandaa kikosi chake kwa lengo la kuhakikisha usiku huu wanavunja mwiko wa kupoteza wanapokua wageni wa jeshi hilo la Ashburton Grove.

Mancini pia akazizungumzia klabu nyingine ambazo zina nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu lakini bado wakaendelea kushikilia msimamo wake wa kufanya maajabu msimu huu licha ya baadhi ya klabu kukiri zina uwezo mkubwa dhidi ya Man City.

Michezo mingine ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza inayochezwa usiku huu ni pamoja na:

Villa Park.
Aston Villa v Sunderland

St James Park.
Newcastle v West Ham

Ewood Park.
Blackburn v Liverpool

Reebok Stadium.
Bolton v Wigan

No comments:

Post a Comment