KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, January 5, 2011

SPURS SI ILE YA MIAKA YA NYUMA.


Huko Goodson Park, Napo joto la mchezo wa hii leo kati ya wenyeji Everton dhidi ya Tottenham Hotspurs limepanda kwa kiwango cha hali ya juu kufuatia meneja wa The Toffees David Moyes kuwazungumzia kwa undani wagani wao.

Moyes amepata nafasi ya kuzungumza na vyombo vya habari na kueleza kwamba Spurs wanayokwenda kucheza nayo usiku huu si Spurs ya miaka ya nyuma hivyo wamejitayarisha kwa lolote ambalo linaweza kujitokeza, lakini ukweli ni kwamba bado kikosi chake kina nafasi ya kupata ushindi kwa faida ya kucheza nyumbani.

Meneja huyo wa kimataifa toka nchini Scotland amesema hana cha kuhofia dhidi ya wapinzani wake lakini bado akaendelea kukumbusha umahiri wa Spurs msimu huu ambao umeshuhudia wakipata nafasi ya kucheza na klabu kubwa barani Ulaya kama Inter Milan kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya na kuonyesha hali ya ukomavu wa kisawa sawa.

Spurs wanakwenda kucheza mchezo wa usiku huu huku wakiwa na kumbu kumbu ya ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata mwishoni mwa juma lililopita mbele ya Fulham ambao walikubali kisago cha bao moja kwa sifuri lililopachikwa na winga machachari Garethe Bale.

No comments:

Post a Comment