KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, January 8, 2011

ZOGO LAIBNUKA FAINALI ZA MWAKA 2022.


Siku moja baada ya raisi wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter kuonyesha hatua ya kuyaunga mkono maombi ya viongozi wa soka huko Barani Asia ya kutaka fainali za kombe la dunia mwaka 2022 zichezwe mwezi januari na si kati kati ya mwaka kama ilivyo kawaida, mameneja wa vilabu nchini Uingereza wamepinga hatua hiyo.

Mameneja hao kwa nyakati tofauti wamesema utaratibu huo endapo utakubaliwa na shirikisho la soka duniani FIFA utaharibu mfumo wa ligi sambamba na kuleta malumbano kati ya vilabu na nchi shirikia ambazo zitawahitaji wachezaji wao mapema kwa ajili ya maandalizi ya fainali hizo za mwaka 2022.

Mameneja hao waliopinga hatua hiyo ni Mark Hughes wa Fulham, Harry Redknapp wa Spurs, Arsene Wenger wa Arsenal pamoja na kocha mkuu wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Graham Taylor.

Mbali na malalamiko hayo Arsene Wenger amesema kwa upande mwingine huenda ikawafurahisha Waingereza kutoka nje ya nchi yao kwenda kutazama fainali za kombe la dunia mara baada ya pilika pili za sikuu za mwishoni mwa mwaka, lakini mbali na hivyo bado matatizo kadha wa kadha ya mfumo wa msimu wa soka yatajitokeza.

Wakati hatua hiyo ya kupinga ikijitokeza miongoni mwa maweneja wa soka nchini Uingereza, raisi wa chama cha soka nchini Qatar Mohammed Bin Hammam amesema mikakati ya kutaka kuzihamisha fainali hizo kutoka mwezi June ama July na kuzirejesha nyuma hadi mwezi januari hazijafanywa na nchi yao hivyo amewataka mashabiki wote ulimwenguni kuelewa hivyo.

Amesema wao walikua tayari na wapo tayari kuandaa fainali hizo mwezi June ama July kama ilivyo kawaida kutokana na kuwa maandalizi ya kukabiliana na hali ya joto yatakayofanywa, lakini hawana budi kusubiri nini kitakachoamuliwa, baada ya viongozi wa soka barani Asia kuwakilisha maombi ya kurejeshwa nyuma kwa fainali hizo.

Kama nilivyokueleza hapo awali raisi wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter yeye ndie chanzo cha malumbano haya yaliyojitokeza kuafutia kauli aliyoitoa jana mbele ya waandishi wa habarti nchini Qatar ambapo alisema yeye binafsi anakubali fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 zichezwe katika msimu wa majira ya baridi huko Falme za kiarabu.

Amesema sababu kubwa ya kufikiria hivyo kwa mawazo yake binafsi ni huruma kwa wachezaji na si kwa mashabiki hivyo bado anaamini suala hilo lina uzito wa aina yake pale kamati kuu ya FIFA itakapokutana kulijadili na muafaka kutolewa.

Wakati huo huo fainali za mataifa ya barani Asia jana zimefunguliwa rasmi mjini Doha nchini Qatar, kwa kushuhudia mchezo kati ya wenyeji Qatar dhidi ya Uzbekistan.

Matokeo ya mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa kimataifa wa Khalifa, ni kwamba wenyeji timu ya taifa ya Qatar walilala kwa idadi ta mabao mawili kwa sifuri yaliyofungwa na Odil Ahmedov pamoja na Server Djeparov katika dakika ya 59 na 77


No comments:

Post a Comment