KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 31, 2011

AFRIKA KUSINI KUOMBA UENYEJI WA 2014.


Aliekua mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2010, Daniel Alexander Jordaan, amesema nchi ya Afrika kusini inajiandaa kuwasilisha maombi ya kuandaa fainali za klabu bingwa duniani za mwaka 2014.

Daniel Alexander Jordaan ambae anawania nafasi ya ujumbe ndani ya shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA ameyazungumza hayo alipokua mjini Lubumbashi huko Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, baada ya kikao cha kamati ya utendaji ya CAF ambayo ilikutana mjini humo kuamua nani atakua mwenyeji wa fainali za mataifa ya bara la Afrika kwa mwaka 2015 na 2017.

Amesema wanaimani maombi ya nchi hiyo yatafanikiwa hasa ukizingatiwa nchi ya Afrika kusini ina vigezo vyote vinavyotakiwa katika utaratibu wa kuandaa fainali kubwa za soka duniani baada ya kufanikiwa kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010.

Amesema umewadia wakati sasa kwa bara zima la Afrika kujitangaza kwa kutumia faida zilizopo barani humo, kwa kutumia mikakati ya nchi fulani ambayo itaweza kufikia malengo yaliyowekwa na CAF katika kukuza soka.

No comments:

Post a Comment