KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, January 31, 2011

Luis Javier García Sanz ATOA MSUKUMO WA TORRES KUONDOKA.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Hispania pamoja na klabu ya Panathinaikos ya nchini Ugiriki Luis Javier García Sanz ameunga mkono hatua ya mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Hispania Fernando José Torres Sanz ya kutaka kuondoka huko Anfield na kujiunga na klabu ya Chelsea.

Luis Javier García Sanz ameunga mkono hatua hiyo kufuatia kauli yake aliyoizungumza ambapo amesema umewadia wakati kwa mshambuliaji huyo kubadili mazinigira na kusaka sehemu nyingine mbali na Liverpool alipodumu kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

Amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, bado ana kiu ya kupata mafanikio akiwa na klabu mpya baada ya kusubiri kwa muda mrefu huko Anfield lakini kwa bahati mbaya mafanikio hayo yameshindwa kupatikana hasa kutwaa ubingwa wa soka wa nchini Uingereza sambamba na kucheza ligi ya mambingwa barani Ulaya msimu ujao baada ya kukosa msimu huu.

Hata hivyo Luis Javier García Sanz amekiri kushtushwa na taarifa hizo za Torres kutaka kuihama klabu ya Liverpool ambayo tayari ameshakiri kuihusudu kutoka moyoni mwake.

Luis Javier García Sanz pia ametoa angalizo kwa mshambuliaji huyo kwa kusema kwamba kuelekea kwake Chelsea bado kutakua ni kitendawili cha kutatua tatizo la klabu hiyo ama kushindwa kutatua tatizo hivyo anatakiwa kuwa macho na kutambua uwepo wake ndani Stamforde Bridge endapo atafanikiwa kuhama usiku huu.

Kiungo huyo ambae pia alishawahi kuitumikia klabu ya Liverpool kuanzia mwaka 2004-07 amebainisha wazi kwamba alibahatika kukutana na Torres wakiwa nchini Hispania na hakuwahi kumueleza suala lolote juu ya kutaka kuondoka Liverpool zaidi ya kumsisitizia mapenzi yake dhidi ya klabu hiyo ya Meceyside.

Wakati huo huo meneja wa klabu ya Liverpool KING KENNY DALGLISH ameendelea kutoa msisitizo wa kutomuuza Fernando José Torres Sanz huku akibainisha wazi kwamba kusajiliwa kwa Luis Alberto Suárez Díaz kutoka Ajax Amsterdam hakumaanishi mshambuliaji huyo amekwenda Anfield kuziba nafasi ya mspaniola huyo.

King Kenny amethibitisha kwamba atapigana kufa na kuponda ndani ya kipindi cha saa kadhaa zilizosalia kuhakikisha mshambuliaji huyo haondoki katika himaya yake ambayo sasa tayari imeshaanza kuonekana kutengemaa na kuyakaribia mafanikio yaliyowekwa ya kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi.

No comments:

Post a Comment