KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, February 26, 2011

Alessandro Del Piero KUENDELEA NA JUVENTUS.


Mshambuliaji wa kimataita toka nchini Italia Alessandro Del Piero amekubalia kusaini mkataba maalum na uongozi wa klabu yake ya Juventus ambao utamuwezesha kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa muda wa mwaka mmoja ujao.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amekubali kusaini mkataba huo maalum, kwa lengo la kuendelea kuwaridhisha viongozi pamoja na mashabiki wake ambao bado wanatamani kumuona akiendelea kuwepo huko Stadio del Alpi.

Mkataba huo umejumuisha masuala muhimu kati ya Alessandro Del Piero dhidi ya viongozi wake ambao bado watakuwa na nafasi nyingine ya kumuongezea chochote kitu pale atakapofikia melngo wanayoyahitaji.

Akizungumza kupitia televisheni ya klabu hiyo ya nchini Italia Alessandro Del Piero amesema mkataba aliousaini umejumuisha masuala mengi ambayo ni ya siri hivyo ataendelea kuwepo klabuni hapo kama wengi walivyokua wakihitaji.

Amesema mbali na kusaini mkataba huo pia huenda akasaini mkataba mwingine ambao utamuwezesha kuvaa jezi isiyo an maandishi yoyote ya klabu ya Juventus ambayo kwa hivi sasa ina maandishi ya kampuni inayotengeneza vyakula vya wanga nchini italia.

Alessandro Del Piero mpaka sasa ameshaitumikia klabu ya Juventus 667 na amefanikiwa kufunga maboa 280 toka alipojiunga na Juventus mwaka 1993 akitokea Calcio Padova FC.

No comments:

Post a Comment