KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, February 26, 2011

NI SHUGHULI PEVU KESHO !!!


Siku moja kabla ya mtanange wa hatua ya fainali ya kombe la ligi huko nchini Uingereza *Curling Cup* haujapigwa huko jijini London katika uwanja wa Wimbely tambo zimeanza kusikika kutoka pande zote mbili zinazowania ubingwa wa michuano hiyo ambazo ni Arsenal pamoja na Birmingham city.

Birmingham City ambao walitinga katika hatua hiyo baada ya kuwabanjua wapinzani wao wakubwa katika jiji la Birmingham Aston Villa wametoa tambo zao kupitai kwa meneja Alexander "Alex" McLeish ambae amekiri mchezo huo ni muhimu sana kwake toka alipoanza kufanya kazi nchini Uingereza mwaka 2007.

Alexander "Alex" McLeish amesema kutokana na sababu hiyo hana budi kufanya jitihada binafsi ambazo zitamuwezesha kuwashinda wapinzani wake Arsenal hiyo kesho kwa lengo la kupata mafanikio yake ya kwanza ya kutwaa ubingwa akiw akatika ardhi ya Uingereza.

Amesema mbali na kutambua umuhimu wa mchezo huo pia kikosi chake pamoja na mashabiki wana faida ya kucheza na kushudia mchezo huo wakiwa katika uwanja huru.

Hata hivyo Alexander "Alex" McLeish amesema anatambua hiyo kesho wamnakwenda kucheza na klabu yenye ukame wa miaka sita wa kutwaa ubingwa hivyo sababu hiyo itakua chachu ya kuongeza ushindani kwa namna yoyote ile.

Amesema naamini wachezaji wake endapo watafanya kile atakachowaomba hiyo kesho wana uwezo mkubwa wa kutwaa ubingwa wa michuamno hiyo na kuweka historia ya kipekee huko St Andrew's.

Nae meneja wa klabu ya Arsenal Arsène Charles Ernest Wenger amesema kikosi chake kipo tayari na haoni sababu ya kuingia uwanjani hiyo kesho huku wakiwa na uwoga wa kuwahofia wapinzani wao ambao tayari wameshakutana nao kwenye michezo yote miwili ya ligi ya kufanikiwa kuwashinda.

Amesema Anatambua kikosi chake kinatazamwa kwa macho mawili kufuatia harakati za kutaka kumaliza ukame unaowakabili, lakini bado akawakumbusha mashabiki kwamba lolote laweza kutokea hivyo wanachotakiwa ni kukubaliana nayo.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 61 ameongeza kwamba atawahimiza wachezaji wake kucheza kwa kujituma zaidi licha ya kutambua suala hilo ni hatari sana kwao kutokana na kuendelea kuwepo kwenye utaratibu wa kusaka ubingwa wa michuano mingine msimu huu.

No comments:

Post a Comment