
Kiungo wa kimataifa toka nchini Urusi Andrey Arshavin ameripotiwa yu katika wakati mzuri wa kujitenegenezea mazingira ya kurejesha heshima kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal, baada ya klabu hiyo kuikataa ofa ya klabu yake ya zamani ya Zenit St Petersburg iliyokua imepania kumrejesha nyumbani mwezi januari mwaka huu.
Andrey Arshavin ameripotiwa kuwa katika mazingira hayo, kufuatia kuonyesha kiwango duni toka msimu huu ulipoanza hivyo amedhamiria kufanya jitihada za kurejea katika kiwango chake kama ilivyokua siku za nyuma alipoelekea huko jijini London.
Rafiki wa karibu wa mchezaji huyo wamekaririwa na vyombo vya habari wakisema kwamba Andrey Arshavin mara nyingi amekua akiwaeleza ni vipi alivyopania kurejea katika kiwango chake na kumridhisha meneja Arsene Wenger ambae bado anaamini anaweza kufanya hivyo.
Toka msimu huu ulipoanza Andrey Arshavin ameshacheza michezo 34 ya michuano yote na amefanikiwa kupachika mabao manane.
No comments:
Post a Comment