
Kampuni ya Olympic Park Legacy (OPLC), ambayo ina jukumu la kuamua ni nani atakae umiliki uwanja wa Olympic wa jijini London kati ya vilabu viwili vya West Ham Utd pamoja na Tottenham Hotspurs, hii leo itatoa jibu rasmi la nani ameibuka kidedea kufuatia maombi yaliyowasilishwa mezani miezi kadhaa iliyopita.
Kinyang’anyiro hicho kinatarajia kufikia kikomo hii leo huku vilabu hivyo vikiwa na matumaini makubwa ya kila mmoja kumshinda mwenzake kufuatia kujiamini kwa sifa zilizoainishwa kwenye maombi yao.
Hata hivyo toka siku ya jumatano taarifa zimekua zikieleza kwamba uwanjani huo huenda ukakabidhiwa kwa klabu ya West Ham Utd kufuatia sifa yao kubwa inayoendelea kuwabeba ya kutoondoa sehemu ya kukimbilia mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Olympic ya mwaka 2012 ili hali wapinzani wao Spurs wameshaainisha kwamba sehemu hiyo itaondolewa endapo watashinda.
Vilabu hivyo viwili vinawania kuumiliki uwanjani huo kutokana na kuwa na mipango ya kutaka kuvihama viwanja vayo vya sasa huku kila mmoja akidai kwamba sababu kubwa ni kutaka kutoa nafasi kwa mashabiki wengi wa vilavu hivyo kuzishuhudia timu zao kwa nafasi.
Klabu yoyote itakayotangazwa kushinda katika kinyang’anyiro hicho hii leo, itakabidhiwa uwanjani huo mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Olympic ya mwaka 2012 iliyopangwa kufanyika jijini London, lakini bado serikali ya nchini uingereza itakua na nguvu za kuumiliki uwanja huo.
No comments:
Post a Comment