
Beki mpya wa klabu ya Chelsea David Luiz ametambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari mara baada ya kusajiliwa klabuni hapo mwishoni mwa mwezi uliopita akitokea kwenye klabu ya Benfica ya nchini Ureno.
Beki huyo wa kimataifa toka nchini Brazil, ametambulishwa, huku ikiwa tayari ameshaitumikia klabu hiyo katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Liverpool walioondoka na ushindi wa vbao moja kwa sifuri huko Anfield.
Utambulisho wa David Luiz mwenye umri wa miaka 23 umefanywa na meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Michelangelo Ancelotti ambapo mesema kusajiliwa kwa beki huyo kutatoa nafasi ya wachezaji wake wanaocheza katika safu ya ulinzi kupokezana bakle itakapobidi kufanywa hivyo.
No comments:
Post a Comment