KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, February 12, 2011

David Gold AONYESHA FURAHA YAKE BAADA YA KUUPATA UWANJA WA OLYMPIC.


Siku moja baada ya kutangazwa mshindi wa kunyang’anyiro cha kuwani uwanja wa Olympic wa jijini London, mmiliki mwenza wa klabu ya West Ham Utd David Gold ameelezea furaha yake kufuatia bahati hiyo ilioyowaangukia.

Akielezea furaha hiyo nje ya uwanja huo utakaotumika kwa ajili ya michezo ya Olympic ya mwaka 2012, David Gold amesema ni jambo jema kwao kuwa wamiliki wa uwanja huo ambao utafungua ukarasa mpya wa klabu ya West ham Utd ambayo kwa sasa inautumia uwanja wa Upton Park uliopo magharibi mwa jiji la London.

Amesema safari ya kuanza kuutumia uwanja huo ni ndefu lakini kwake anaona kama ni sehemu ya kutoa mwanya kwa wachezaji chipukizi waliopo sasa klabuni hapo kucheza katika uwanja huo maridhawa ambao watakabidhiwa rasmi mara baada ya kumalizika kwa michezo ya Olympic ya mwaka 2012.

Wakati huo huo meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Redknapp ametoa pongezi zake za dhati kwa uongozi, wachezaji pamoja na amshabiki wa klabu ay West Ham Utd kufuatia kuibuka kidedea wa kinyang’anyiro cha kuumiliki uwanja wa Olympic.

Amesema kila mmoja wao alikua na jukumu la kukubaliana na matokeo yaliyotangazwa jana na wao kama Spursd hawana budi kukubalia kushindwa katika ushindani huo uliodumu kwa majuma kadhaa yaliyopita.

No comments:

Post a Comment