
Nchini Uingereza michuano ya kombe la chama cha soka nchini humo FA inaendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja wa marejeano kati ta Bolton Wanderers dhidi ta Wigan Athetics utakaounguruma huko DW Stadium.
Mchezo huo umelazimika kucheza kwa mara ya pili, kufuatia timu hizo mbili kushindwa kufungana katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nne uliochezwa Reebok Stadium mnamo Januari 30
Wigan wanaingia uwanjani hii leo bila ya kuwa na beki wao wa kimataifa toka nchini Uingereza Emmerson Orlando Boyce, kutokana na maumivu wa nyama za paja yanayomsumbua kwa sasa.
Kwa upande wa Bolton Wanderers wao watamkosa beki Zatyiah "Zat" Knight anaesumbuliwa na maumivu wa goti aliyoyapata mwishoni mwa juma lililopita kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Everton.
Pia pande zote mbili nikizungumzia Wigan pamoja na Bolton hazitopruhusiwa kuwatuimia wachezaji waliosajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo la usajili ambao hawakucheza mchezo wa kwanza.
No comments:
Post a Comment