KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, February 16, 2011

Arsenal v Barcelona - UEFA Champions League.



Meneja wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelola Josep "Pep" Guardiola i Sala amewahimiza wachezaji wake kucheza kwa kujituma katika mchezo wa usiku huu ambao unawakutanisha na washika bunduki wa Ashburton Grove Arsenal.

Pep Guardiola amesema endapo wachezaji wake watacheza kwa kuwadharau wapinzani wao kuna kila sababu ya kuonekana kwa mabadiliko makubwa zaidi ya msimu uliopita ambapo walipokwenda huko jijini London kucheza na washika bunduki hao walimaliza kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Amesema Arsenal ni klabu yenye wachezaji wazuri na mara zote wamekua wakicheza bila kuchoka hivyo kama watashindwa kwenda sambamba na kasi ya wapizani wao hawatoweza kutimiza malengo yaliyowapeka huko Emirates.

Meneja huyo wa kimataifa toka nchini Hispania pia amethibitisha kuwa shabiki namba moja wa klabu ya Arsenal ambapo sababu kubwa ya kuvutiwa na klabu hiyo ni soka safi ambalo wamekua wakilionyesha dhidi ya klabu pinzani wanazokutana nazo katika michuano kadha wa kadha kila msimu.

Wakati Josep "Pep" Guardiola i Sala, akithibitisha kuihusudu Arsenal, meneja wa klabu ya Arsenal Arsène Charles Ernest Wenger amesema wachezaji wake usiku huu wastahili kuthibitisha wamebadilika kwa kiasi kikubwa baada ya kuondoshwa na FC Barcelona msimu uliopita katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya ligi ya mabingwa.

Arsène Charles Ernest Wenger amesema wachezaji wake wana haki ya kuthibitisha hilo kutokana na dhana potofu inayoendelea miongoni mwa mashabiki wengi ulimwengu mzima ambayo imekua ikiwafanya kuhisi Arsenal katu hawawezi kuibanjua Barcelona.
Mbali na kuwataka wachezaji wake kuthibitisha hilo linawezekana pia mzee huyo wa kifaransa amezungumzia uwezekano wa kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani ulaya msimu huu kwa upande wa kikosi chake endapo watafanikiwa kufanya kweli na kuiondosha patupu Barcelona.

Nae beki wa kimataifa toka nchini Uswiz ambae ni mzaliwa wa nchini Ivory Coast Johan Danon Djourou-Gbadjere ameeleza wazi kwamba mchezo wa hii leo anauchukulia kama michezo mingine aliyowahi kucheza kiwa na klabu ya Arsenal.

Johan Danon Djourou-Gbadjere ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya kuonogozana na meneja wake Arsene wenger ambapo ameeleza wazi kwamba siku zote anapokua uwanjani huiheshimu klabu yoyote wanayokutana nayo hivyo na Barcelona anaiheshimu pia.

Mbali na kuisemea nafsi yake mwenyewe pia beki huyo mwenye umri wa miaka 24, amezungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake ambapo ametanabai kwa kuwakumbusha mashabiki wanaowabeza kwamba nao wana uwezo wa kuzuia na kushambulia hivyo hakuna namna ya kuuzungumzia upande mmoja.

Mchezo mwingine usiku huu wa michuano hiyo ya ligi ya mabingwa barani ulaya utachezwa huko mjini Roma nchini Italia katika uwanja wa Olimpico mbapo wenyeji AS Roma watakuwa wenyeji wa Shakhtar Donetsk kutoka nchini Ukraine.

No comments:

Post a Comment