
Chama cha soka nchinio Uingereza FA kimetoa onyo kwa wachezaji wa vilabu vya soka nchini humo juu ya matumizi ya mtandao wa kijamiii wa Twitter.
FA wameamua kutoa onyo hilo baada ya kuonekana kwamba kuna baadhi ya wachezaji wa vilabu hivyo wamekua wanautumia vibaya mtandao huo kwa kuandika masuala ya ajabu ambayo hayaendani na mchezo wa soka.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho na kusambazwa katika vilabu vyote, imeeleza kwamba wachezaji wote kuanzia sasa wanatakiwa kuwa na utaratibu wa kuutumia mtandao huo vizuri na yoyote atakaebainika kwenda kinyume na utaratibu uliowekwa adhabu kali itamuangukia kupitia kifungu cha E3 cha kanuni za ligi.
Onyo hilo limetolewa huku FA wakiwa tayari wameshamuadhibu winga wa zamani wa klabu ya Liverpool Ryan Babel kwa kumtoza faini ya paund 10,000 baada ya kuweka picha ya kutengeneza ya muamuzi Howard Webb aliekua amevalia jezi za klabu ya Man Utd, kitendo ambacho kiliashiria refa huyo ni shabiki namba moja wa klabu hiyo ya Old Trafford.
Mbali na sakata hilo, kiungo wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere, nae al-manusura aingie kwenye mkumbo huo, lakini alinusurika baada ya kuuondoa ujumbe wake haraka kwenye mtandao huo uliokua unamkashifu muamuzi aliechezesha pambano kati ya The Gunners dhidi ya Newcastle utd.
No comments:
Post a Comment