
Harakati za jopo la madaktari wa klabu ya Tottenham Hotspurs za kuhakikisha winga wa kimataifa toka nchini Wales Gareth Bale anauwahi mchezo wa hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya AC Milan utakaochezwa kesho huko mjini Milan nchini Italia zimegonga ukuta.
Jopo la madaktari wa klabu hiyo, limekua likijitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha winga huyo anapona maumivu ya mgongo yanayomkabili ndani ya majuma matatu yaliyopita, lakini taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia hii leo na meneja wa klabu ya Spurs Harry Redknapp zimeeleza kwamba Bale hatokuwepo huko San Siro.
Harry Redknapp amesema hawezi kuhatarisha maisha ya winga huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa kumlazimisha kucheza katika mchezo huo mgumu hivyo inamlazimu kusubiri hadi atakapopona kabisa ili aweze kumrejesha kundini hususan katika mchezo wa marudiano dhidi ya Ac Milan utakaochezwa march 9 mwaka huu huko jijini London.
Katika hatua nyingine mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza Peter Crouch nae yupo mashakani kucheza mchezo huo wa kesho kufuatia maumivu ya mgongo yanayomkabili huku kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi Rafael van der Vaart akipewa nafasi finyu ya kucheza kufuatia maumivu ya kigimbi cha mguuu yanayomsumbua.
Nae kiungo wa kimataifa toka nchini Croatia Luka Modric nae anafikiriwa kucheza mpambano huo dhidi ya AC Milan, baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo kutokana na matatizo ya appendix yaliyokua yakimsumbua.
No comments:
Post a Comment