KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, February 25, 2011

FABREGAS KUUKOSA MCHEZO WA FAINALI J2.


Nahodha na kiungo wa klabu ya Arsenal Cesc Fabregas ataukosa mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la ligi utakaochezwa siku ya jumapili kwenye uwanja wa Wimbley uliopo jijini London ambapo Arsenal watapambana na Birmingham City.

Cesc Fabregas ataukosa mchezo huo kufuatia kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja ambayo yalimlazimisha kutolewa nje katika mchezo wa ligi dhidi ya Stoke City uliopigwa usiku wa kuamkia jana huko Emirates Stadium ambapo wenyji walichomoza na ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Charles Ernast Wenger tayari ameshathibitisha taarifa hizo ambapo amesema licha ya kuwa nje siku ya jumapili bado haifahamiki kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani.

Amesema hatua hiyo imemuhuzunisha sana kiungo huyo wa kimataifa toka nchini Hispania ambae tayari alikua amshapania kucheza mchezo huo wa fainali ambao huenda ukamaliza ukame ya kutwaa vikombe ulidumu huko Emirates kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Katika hatua nyingine Arsene Charles Ernast Wenger amesema katika mchezo huo mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uholanzi Robin van Persie, beki wa kimataifa toka nchini ufaransa Laurent Koscielny pamoja na kiungo wa Ufaransa Vassiriki Abou Diaby watarejea kikosini.

No comments:

Post a Comment