KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, February 25, 2011

SUBRA YAENDELEA KUTAWALA.


Mashabiki wa klabu ya Liverpool wenye shauku ya kutaka kumuona mshambuliaji wao mpya Andrew Thomas Andy Carroll akianza kuitumikia klabu hiyo wameendelea kuombwa kuwa watulivu katika kipindi hiki.

Rai hiyo ya utulivu imetolewa na meneja wa klabu hilo King Kenny Dalglish ambapo amesema Andrew Thomas "Andy" Carroll bado anaendelea na matibabu na muda si mrefu ataanza kuonekana kwenye kikosi chake.

King Kenny Dalglish amelazimika kulizungumzia suala la mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kufuatia baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa Andrew Thomas "Andy" Carroll huenda akajumuishwa kikosini katika mchezo wa siku ya jumapili dhidi ya West Ham Utd ambao watakua nyumbani huko Upton park.

Amesema kwa sasa Andrew Thomas "Andy" Carroll anaendelea vyema na ukweli ni kwamba yu karibuni kurejea tena uwanjani kwa lengo la kukitumikia kikosi cha klabu yake ya Liverpool, iliyomsajili akitokea St James Park yalipo makao makuu ya klabu ya Newcastle Utd kwa ada ya uhamisho wa paund million 35.

Wakati huo huo meneja huyo wa kimataifa toka nchini Scotland amekiri kikosi chake usiku wa kuamkia hii leo kilikua na shughuli ya ziada kwa kuhakikisha wanavuka katika hatua ya 32 bora ya michuano ya ligi ya barani ulaya dhidi ya klabu ya Sparta Prague ya jamuhuri ya Czech.

Amesema wachezaji wake kiujumla walicheza kwa kujituma na walitambua umuhimu wa ushindi katika mchezo huo na mwishowe walifanikiwa kupata bao lililowekwa nyavuni na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uholanzi Dirk Kuyt.

Ushindi huo wa bao moja kwa sifuri umeipa nafasi klabu ya lIverpool kutinga kwenye hatuaya 16 bora ya michuano ya kombe la ligi barani ulaya ambapo sasa watakutana na Sporting Braga kutoka nchini Ureno.

No comments:

Post a Comment