KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, February 16, 2011

KAMATI YA NIDHAMU KUMJADILI GATUSO.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Italia na klabu ya AC Milan Gennaro Ivan "Rino" Gattuso huenda akahukumiwa kifungo cha muda mrefu na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kufuatia vitendo vya utovu wa nidhamu alivyomfanyia meneja msaidizi wa klabu ya Tottenham Hotspurs Joe Jordan.

Gennaro Ivan "Rino" Gattuso anafikiriwa kuingia katika kifungo hicho cha muda mrefu huku uongozi wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA ukitangaza kuwa kamati ya nidhamu itakutaka mwanzoni mwa juma lijalo kujadili suala hilo.

Gattuso ambae jana alikiongoza kikosi cha Ac Milan akiwa kama nahodha alionyesha vitendo hivyo mara mbili ambapo kwa mara ya kwanza alimsukuma meneja huyo msaidizi wa klabu ya Spurs Joe Jordan shingoni na kisha mara baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa kiungo huyo alirejea kitendo hicho kwa kumsukuma kwa kichwa.

Hata hivyo tayari Gennaro Ivan Gattuso ameomba radhi kwa kitendo hicho alichokifanya katika mchezo wa jana wa hatua ya 16 bora wa michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Spurs ambapo amesema tukio hilo alilifanya kwa bahati mbaya.

Amesema alidiriki kufanya hivyo kutokana uhalisia wa mchezo huo wa jana ambao ulitawaliwa na upinzani wa hapa na kule hivyo kwa sasa anajutia kosa alilolifanya.

Gatuso amesema kabla ya kufanya kitendo cha kumsukuma Jordan kwa mara ya kwanza alikua akizungumza nae lugha ya Scotish ambayo amegoma kuzungumza alichomueleza mzee huyo na mwisho wa siku alishindwa kuvumilia na kuamua kutimiza kile kilichoonekana.

Hata hivyo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 amesema yu tayari kukubaliana na adhabu yoyote itakayomuangukia mara baada ya kuhitimishwa kwa kikao cha kamati ya nidhamu ya UEFA juma lijalo.

Wakati huo huo meneja wa klabu ya Tottenham Hotsours Harry Redknapp ameonyesha kuchukizwa na tabia ya Gennaro Ivan "Rino" Gattuso ambayo ameiita ni ya kipumbavu na wala haipaswi kuvumiliwa na viongozi wa juu wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.

Amesema mchezaji huyo hana adabu ya kuheshimu mchezo wa soka ambao ndio maisha yake na kwa sasa hana budi kuadhibiwa kwa makosa ya kipuuzi aliyoyafanya hapo jana.

Pia meneja huyo wa kiingereza amezungumzia kuchukizwa na maamuzi ya muamuzi aliechezeha pambano la jana Stephane Lannoy kutoka nchini Ufaransa baada ya kushindwa kumuadhibu kwa kumuonyesha kadi nyekundu kiungo wa Ac Milan Mathew Flamin baada ya kumchezea ovyo beki wake wa kulia Vladmir Corluca.

No comments:

Post a Comment